#muhitimu: Sehemu ya 1
"Raha jipe mwenyewe"
Nikaifunua
tena karatasi yangu ya mtihani katikati, nikaliangalia lile swali ambalo
sijalichagua kulijibu na likafanikiwa kuvuta akili na hisia zangu, nikaendelea
kulitazama kwa umakini kama nataka kulijibu ila bila wasiwasi wowote kwasababu
nimeshamaliza kujibu maswali matano ya uhakika yanayotakiwa na kuyahakikisha
kama yako sahihi, wasi wasi wa nini?
Liilikua
swali la nne katika ile karatasi ya mtihani, swali la picha au kama liitwavyo
“photograph” kuitizama picha ile kwa makini na kisha kujibu maswali
yaliyoulizwa, kwa mara ya kwanza picha ya hilo swali iliewekewa rangi katika
mtihani wa kidato cha sita. Swali likaendelea kunivuta, japo sikuhitaji
kulijibu lakini nilipendezwa sana na picha ya swali hilo.
Ilikua ni picha
ya ufukwe mmoja sijui ni wa wapi ila nadhani ni hapa hapa Tanzania, mchanga
mwingi, mzuri na laini uliyatenganisha maji na nchi kavu na juu ya ule mchanga
kulikua na mstari wa vibanda vya kupumzikia kama 'viduku' ambavyo viliweka kivuli
safi, vilikua vya nguzo ya wastani iliyoezekwa kwa majani juu, na chini ya kila
kimoja palikua na kiti kama kitanda kidogo kwa ajili ya kujilaza. Mwisho kabisa
mwa picha kulikua na watu walioonekana kwa mbali ‘wakila raha’ matumbo nje na
hao ndiyo walionivutia.
“Raha jipe
mwenyewe” nilikua katika fukwe za malaika siku mbili baada ya mtihani
nimejipumzisha juu ya mchanga laini kabisa, miguu inaguswa na mawimbi ya maji
yaliyokuwa yanakuja na kuondoka pale ufukweni tulipokaa, sikuwa pekeyangu na pembeni yangu
nilikuwa na jirani yangu ambaye tuliongozana mahali pale na tangu tufike alifanikiwa
kuyavuta macho ya jamaa iliyofika pale pamoja nasi. Mimi na yule mototo mzuri
tulikaa chini ya kivuri kizuri kama vile vijumba vya kwenye mtihani wa jografia
tukijiliwaza kwa soda baridi za kopo, biskuti, bajia na vinyama choma
tulivyokumbuka kuchukua, tulikua tunatoa uchovu wa mitihani mimi na mama yenu
mdogo.
Nikawa naitizama ile miguu yake iliyofunikwa na mtandio uliolowana na sidiria ambayo kama ilikuwa inasukumwa itoke nikawa naona tofauti yangu na wengine ni mimi nilingalia vitu vyangu kwa uhakika wao walikuwa wanachungulia kwa kuibia.
“Ten
minitues to time” alinishtua msimamizi akitaja muda uliyobaki tumalize mtihani,
na kama nilivyoanza nikahitimisha tena kwa sala nikimshukuru Mungu kwa
kuumaliza salama na pia kuomba matokeo mazuri kulingana na jitihada nilizoweka,
yaani niliomba nivune nilichopanda. Nikakusanya vitu vyangu, vidogo nikaweka
mfukoni, vikubwa nikashika kushoto pamoja na karatasi ya mtihani alafu ya
kujibia nikashika kulia nikasimama kwenda kukusanya huku nawaza raha nilizokuwa napata bichi.
............................... itaendelea
Comments
Post a Comment