Line yangu
"Kudadeki"
“Nyota njema huonekana asubuhi” na nilishaanza kuhisi leo nimeziona mbili. Nilipoamka tu nikainama nikachukua simu yangu chini, nikataka niende kwenye mitandao ya kijamii, nikagusa Whatsapp nikakuta hakuna kipya nikakumbuka sina bando. Nikajigeuza upande wa pili nijaribu tena kusinzia nilipotulia tu akili ikaniambia “tumia simu wewe tumeashaamka”
Mara hii nikaishika simu yangu iliyokuwa pale pale kitandani huku nafikiri napataje bandooo, nikakumbuka haitoi mlio ikiingiza meseji nikafagia kutafuta sehemu ya meseji na huko ndiko siku yangu ilikoanzia.
Nikakutana na meseji mbili zote kutoka sehemu moja, nikafungua nikakuta ni miamala kutoka sehemu tofauti, mmoja wa kwa rafiki yangu nilikuwa namdai muda sasa hadi nimeacha, mwingine kwa muhindi mkeka wangu wa wiki mbili ulikuwa umetiki na nilishausahau.
“Acha presha, acha presha dogo” nikajiambia moyoni, nikaona sasa nitulie nione hii pesa yote naitumiaje, nikaachana nayo kwanza.
Nikakurupuka kitandani kama umerushwa nyoka pale nadhani kwasababu ya furaha, nikaingia chooni, nikatoka nikaenda mpaka sebuleni, nilipokaa tu nikagundua sina cha kufanya pela nikaenda jikoni nikakuta panatakiwa kusafishwa nikaingiwa na uvivu na njaa ikaisha. “mi sipiki” nikajiambia kwa kiburi.
Wakati narudi kwenye kochi ndipo nikagundua nyumba yote inatakiwa kufanyiwa usafi nikakata tamaa Zaidi. “Ah ntachelewa kazini, chai ntakunywa mbele huko” nikajisemesha huku nakumbuka ile miamala yangu na ikanitia nguvu za kwenda kuoga nitoke kuelekea ofisini.
Wakati nafunga mlango kutoka nikakumbuka kumjulisha yule jamaa kwamba nimeona muamala wake, nikachukua simu kumpigia huku namalizia kufunga vifungo vya shati wakati natembea taratibu kwa mbali nikamsikia yule mdada anyesemaga haipatikani au inatumika, sikujali nikakumbuka ntakuwa sina dakika, nikajiunga na kifurushi kikagoma, nikasimama kidogo huku akili imeanza kunikaa sawa, nikaenda kwenye meseji labda nimeambiwa chochote, sikuona kitu nikamkumbuka yule mdada aliyenijibu wakati namtafuta yule jamaa.
Nikapiga tena ile namba na mara hii nikaweka sauti kubwa hata nisiamini masikio yangu.
“Ndugu mteja namba yako imefungiwa kwa kuto kukamilisha”
“Mfyuuu” nikafyonza huku nakata asiendelee kunichafulia masikio mimi, nikaviangalia vile vibanda vya mawakala, nikasita kidogo alafu nikaendela kwenda kituoni.
Nikapanda gari la kuelekea ofisi za mtandao wangu wa simu.

Comments
Post a Comment